Wednesday, February 20, 2013

KICHUPA KIPYA TOKA KWA OCHU SHEGGY


Studios za Emptysoulz Production zimeondoa ukimya toka swala la kuhama toka Analog kwenda Digital kuharibu mipango mingi haswa kwa Wasanii, Makampuni mbalimbali na jamii nzima.

Akiongea kwa njia ya simu The C.E.O na Diretor wa Studio hizo bwana Solomon Lamba alilonga na Kazikali kuwa kazi inayotoka kwa sasa ni ya Ochu Sheggy inayokwenda kwa Jina la Kingereza akiwa amepewa mkono na mwanadada Aneth.

Muzic Video hiyo ambayo imefanyika nje ya mji ili kubadili muonekano ili kwenda sawa na Story nzima imeshakamilika na soon wengi wataishuhudia kazi hiyo makini.












Tuesday, February 12, 2013

SIRTINO AKESHA SEDUCTIVE RECORDS


Msanii Sirtino yupo mbioni kutoa Track yake mpya atakayemshirikisha Mr. Blue a.k.a Baisa
Sirtino kwa sasa anaetesa na Single yake ya 2lia haswa katika Luninga amesema watu wakae mkao wa ujio mpya kwani Producer wake Mr. T Touchez amempa kazi kubwa sana kwa kumpa Beat kali hivyo ni lazima aitendee haki Beat hiyo kwa Vocals zenye kumtoa nyoka pangoni.
DIRECTOR WA KITAMBO


Ukisikia kina TMK Wanaume, Dully Sykes ,  Juma Nature, Matonya , Yp , Ydash, Chidi Benz, Tunda man, Madee, Chege na Temba na wengine wengi.... Basi huyu jamaa kapiga Videos kitambo na Mpaka sasa anaendelea gonga Vichupa vikali kwenda mbele.

Kwa jina anaitwa Solomon Lamba na ndiye C.E.O wa Studios za Emptysoulz Production zilizopo Mikocheni karibu na kituo cha mabasi cha ITV.

Ameshawahi beba Kili Awards mara mbili na nyingine toka nje ya nchi, kwa sasa anapiga si kazi za Music Videos tu bali mpaka Tv Programes, Documentarys, na soon anaingia upande wa Movies.

Kazikali imeona si haki kama haitampongeza Director huyu kwa Mchango wake mkubwa ktk Bongo Fleva na Sanaa kwa Ujumla.