Thursday, March 7, 2013

DIAMOND ATINGA SEDUCTIVE KWA MR. TOUCHEZ

Jana Niliweza kupata appointment ya kuingia Studio za Seductive Records pale Mitaa ya Mikocheni Viwandani karibu na kituo cha ITV cha mabasi.

Cha kwanza nilikaribishwa na Walinzi walio makini na kujiandikisha katika kitabu cha wageni na kisha kusachiwa kama kuna chochote kibaya nimebeba then nilipewa go ahead na kuelekea moja kwa moja katika mapokezi nako nilipokewa kwa smile na kusubiri kidogo kwa ndani bado jamaa walikuwa wakipiga kazi.

Baada ya kama nusu saa ndipo sauti tamu ya dada wa mapokezi ilisikika ikisema welcome to seductive na naamini wewe ni mgeni wa T......, nami niliitikia kisha nikajuwa naingia ndani, kumbe ilikuwa ni maswala ya drinks nk nami nikaona safi nikaagiza joice baridi.

Haikupita mda mrefu nikasikia sauti ileile ikiniita tena niingie Studio Lab, ndipo nami nikajisukuma fasta.

Nilipokewa kwa uchangamfu na Mr. T touchez ( Producer ) kisha kukaa kimya na kuangalia jinsi gani mambo yanavyo kwenda katika upikaji wa Single ambayo ni gumzo la mji kwa sasa ya Diamond na Nay.






No comments:

Post a Comment